Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Yesu hakuja kuleta wokovu kwa Wayahudi tu bali kwa wanadamu wote! Sasa aliona dalili kwamba muda umefika atakapokufa kwa ajili ya wote. Maana waliotaka kumwona ni Wayunani, yaani, wacha Mungu ambao kwa asili sio Wayahudi (m.20-24). Tendo la Mariamu vilevile lilikuwa dalili kwa Yesu kwamba kifo chake kinakaribia. Ndiyo maana Yesu alisema, Mwache aiweke kwa siku ya maziko yangu. Kwa maana maskini mnao sikuzote pamoja nanyi; bali mimi hamnami sikuzote (m.7-8). Yesu ni ile chembe ya ngano itakayokufa ardhini ili kutoa mazao mengi. Yaani kifo chake msalabani kitaleta wokovu kwa watu wote. Ndivyo anavyosema Yesu, Nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu (m.32)! Pia kwako msomaji!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/