Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Yuda kutoka nje kunamfanya Yesu aseme, Sasa ametukuzwa Mwana wa Adamu, naye Mungu ametukuzwa ndani yake (m.31). Kwa nini? Kwa sababu kukamatwa kwa Yesu kumekaribia sana kutokana na kazi ya Yuda kumsaliti. Na njia ya Yesu kutukuzwa ni kifo cha msalaba. Yesu amenawisha miguu ya wanafunzi wake, na sasa atakwenda kutoa uhai wake kwa ajili yao. Na anataka wafuate mfano wake: Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi (m.34). Zingitia neno hili kwa kulilinganisha na 1 Yoh 3:16-18: Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu. Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo? Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/