Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Mambo mawili ni wazi: 1. Kwa kila anayemwamini Yesu kumeandaliwa mahali kwa Mungu Baba Mbinguni (m.2-3,Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo)! Yesu anasisitiza: Mna makao mengi. Yaani, usiwe na mashaka! Ameshaandaa mahali kipekee kwa ajili yako. Ni kama ilivyo hapa duniani unapoalikwa kwenye sherehe. 2. Njia ya kufika Mbinguni ni moja! Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi (m.6). Mtu asipokubali kumkiri Yesu Kristo alivyoshuhudiwa katika Biblia, hawezi kuingia uzimani. Maana hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo (Mdo 4:12)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/