Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023

SIKU 28 YA 31

Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe (m.11). Furaha ni jambo muhimu na la msingi katika Ukristo. Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini (Flp 4:4)! Itakuwaje furaha ya Yesu kuwa ndani yetu? 1. Kwa kuutambua upendo wake kwetu na kuupokea (m.9 na 12-13, Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu. ... Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi. Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake). 2. Kwa kutambua hivyo tutatiwa furaha ya kuzitii amri zake na kuzifuata, na kufanya hivyo kutazidisha tu furaha yetu (m.10, Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake). Ni amri kama hii: Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi (m.12 na 17). Tukishapokea upendo wake, yaani wokovu wake, twapata moyo mpya unaompenda Yesu na amri zake.

siku 27siku 29

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023

Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/