Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Yesu alifundisha wazi kwamba katika kumfuata yeye, pia kuna mambo magumu. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu ... kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia (m.19). Ndivyo inavyotokea k.m. mtu akiokoka na kuachana na pombe. Inawezekana kabisa kwamba waliozoea kushiriki naye kilabuni watamchukia na kumwudhi kutokana na msimamo wake mpya. Hali hiyo ni msalaba kwa Mkristo, na majaribu. Ndivyo Yesu alivyowaambia wanafunzi wake akisema, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona (Mt 16:24-25).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/