Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Yesu amefundisha kwamba kulishika neno lake ni dalili ya kumpenda: Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka (14:23-24). Wakati Yesu alipokuwa anasisitiza hivyo, maneno yake yalikuwa bado hayajaandikwa. Swali linakuja: Neno la Yesu ni lipi? Ni lipi lile neno tunalotakiwa kulishika? Katika somo la leo Yesu hutupa jibu la swali hili: Huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu ... atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia (m.26). Katika maandiko ya Mitume, yaani Agano Jipya, twaona jinsi Yesu alivyoitimiza ahadi aliyowapa!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/