Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
“Bado kitambo kidogo” ni maneno yatumikayo mara saba katika somo hili. Yaweza kuwa na maana tano tofauti. Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni (m.16) inaweza kuwa na maana kwamba Yesu atakufa au atapaa kwenda Mbinguni kwa Baba (m.5, 10, 20 na 21). Tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona inaweza kumaanisha kwamba Yesu atafufuka au Roho Mtakatifu atakuja na kumfunua Yesu kwetu. Kisha inaweza kuwa na maana ya kurudi kwa Yesu mara ya pili katika utukufu (m.21-24). Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi (Yn 20:20).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/