Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Ni ajabu sana kwamba njia ya Yesu kutukuzwa ni kifo cha msalaba (mistari yote ya 23-24, 27-28 na 32-34 inaonyesha hiyo)! Ni ajabu, maana kifo cha msalaba kilikuwa cha aibu kabisa. Kwanza, ni wahalifu wabaya waliohukumiwa hivyo. Pili, walisulibiwa wakiwa karibu uchi. Tatu, mateso yao yalikuwa makali sana kupita njia nyingine za kuhukumiwa kifo. Siri ya Yesu alivyofanya ni upendo na utii. Katika Flp 2:6-8 imefafanuliwa hivi,Yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Yesu alikufa badala ya wengine akitimiza mapenzi ya Baba yake! Je, umeuona utukufu wake? Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu (Yn 1:29)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/