Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Mungu ndiye aliyewafanya Wayahudi wengi kuwa na mioyo migumu: Amewapofusha macho, Ameifanya mizito mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao (m.40). Aliyotabiri nabii Isaya yakatimizwa. Na wale viongozi walioamini hawakukiri kwa wazi, kwa maana walipenda utukufu wa wanadamu kuliko utukufu wa Mungu (m.42f). Lakini mtu anayetaka kuwa mfuasi wa Yesu kwa siri, yuko hatarini kupoteza imani yake.Zingatia Neno hili: Kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni. Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni ( Mt 10:32-33). Je, kwako ni muhimu zaidi kupata sifa kwa nani?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/