Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Wengi wahangaika, wakijitaabisha kwa kujenga maisha yao ya Kikristo. Lakini ni Mungu mwenyewe anayetutakasa (m.23, Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo). Basi tumwachie, maana yeye ni mwaminifu ambaye atuita, naye atafanya (m.24), tukikaa karibu naye kwa njia ya Neno lake na maombi. Kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu (1 Yoh 3:3). Busu takatifu (m.26) ambalo walibusiana shavuni na paji la uso wanaume kwa wanaume na wanawake kwa wanawake, lilikuwa alama ya kuwa Mungu amewaumba washarika kama familia katika Kristo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/