Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Bwana Yesu aja (3:13, Wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote)! Wakristo washike tumaini hilo, wakikabiliana na kifo. "Kulala" (m.13) hutumiwa na wengi badala ya "kufa", lakini kwa Wakristo lina maana maalumu: Limejaa tumaini la ufufuo. Kama vile Yesu alivyofufuka, vivyo hivyo hao watafufuka, maana imani yao imewaunganisha naye, wamo katika Yesu, kwani Mungu atawaleta pamoja naye (m.14). Angalia upendo ulivyo mkuu kati yao hata ushinde mauti: Yesu (Bwana-arusi) mwenyewe (m.16,Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni) atakuja kuwachukua, nao waumini (Bibi-arusi) watamlaki (m.17, Sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani), wakae pamoja milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo! (m.18).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/