Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Bwana Yesu aja (3:13, Wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote)! Hivyo Wakristo waonywa wazidi kupendana. Hata mioyo yao wenyewe inawasukuma wafanye hivyo, maana Mungu amewapa Roho wake anayewafundisha kupendana (m.9, Katika habari ya upendano, hamna haja niwaandikie; maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana). Pia anawafanya kuwa si wazembe wala waombaji wanaowategemea wengine kwa mahitaji yao, bali wenyewe wafanye kazi kwa uaminifu na bidii kulingana na uwezo wao ili wasiwe na haja ya kitu chochote (m.11-12, Mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza; ili mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu cho chote). Kwa njia hiyo watapata kuwa baraka kwa Wakristo wenzao na hata kwa "walio nje" (m.12), yaani wasioamini, maisha yao hayo yakiwavuta hao wampokee Yesu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/