Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023

SIKU 3 YA 31

Tafakari jinsi nguvu ya Injili ilivyo kuu: Huwapa waipokeao furaha hata wakiwa katika dhiki (1:6, Mkiisha kulipokea neno katika dhiki nyingi, pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu), na kuwapa waihubirio ujasiri wa kuendelea kuieneza hata wakipigwa (m.2, Tukiisha kuteswa kwanza na kutendwa jeuri, kama mjuavyo, katika Filipi, twalithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu) na kuwekwa gerezani kama ilivyokuwa kwa Paulo na Sila (ili kusoma habari zote, angalia Mdo 16:19-25). Ni kwa sababu Injili ni yake Mungu (m.2, Twathubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu). Kwa hiyo Paulo alikuwa mtumishi wa wote kwa ajili ya Yesu. Ndiyo maana anasema, Hatujihubiri wenyewe, bali Kristo Yesu ya kuwa ni Bwana; na sisi wenyewe kuwa tu watumishi wenu kwa ajili ya Yesu (2 Kor 4:5). Maana yake ni kwamba katika kuwatumikia watu alitafuta kibali cha Yesu wala si kibali chao kwa njia ya kuwapendeza. Paulo si kama wapendezao wanadamu, bali wampendezao Mungu anayetupima mioyo yetu (m.4). Tukifuata kielelezo hicho, pia uinjilisti wetu utakuwa na mafanikio mema maana hautakuwa bure (m.1, Maana ninyi wenyewe, ndugu, mwakujua kuingia kwenu, ya kwanza hakukuwa bure).

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023

Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/