Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Injili huleta upinzani kwa sababu ni habari njema na wanadamu ni waovu. Lakini Injili humbadilisha mtumishi wake, kwa hiyo Paulo alikabili upinzani huo kwa moyo mweupe (m.5, Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wo wote, kama mjuavyo, wala maneno ya juujuu ya kuficha choyo; Mungu ni shahidi), akifanya kazi yake kwa ujasiri (2:2, Twalithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu, kwa kuishindania sana) pasipo na nia danganyifu (2:3, Maonyo yetu siyo ya ukosefu, wala ya uchafu, wala ya hila. M.6, Hatukutafuta utukufu kwa wanadamu), bila kutafuta fedha wala heshima (rudia m.5-6), na bila kuchoka, kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu awaye yote (m.9). Hivyo twafunga vinywa vya wapinzani! Tafakari pia jinsi Paulo alivyowapenda Wathesalonike kama watoto wake mwenyewe: Tukikuwa wapole katikati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe. Vivyo hivyo nasi tukiwatumaini kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapa, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu. ... jinsi tulivyomwonya kila mmoja wenu kama baba awaonyavyo watoto wake mwenyewe, tukiwatia moyo (m.7-8 na 11). Upendo huo wa Paulo unatokana na kwamba Mungu alikuwa amewaita wawe watoto wake. Angalia m.12 ambapo Mungu anasifiwa kama mwenye kuwaita ninyi ili mwingie katika ufalme wake na utukufu wake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/