Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano
Nabii anamalizia ujumbe wake kwa kutangaza hukumu ya Mungu itakayowapata wenye kiburi na waovu wasiotaka kusikia na kutii Neno la Mungu. Hukumu inafananishwa na mkulima anayechoma mashamba yake baada ya mavuno. Ni wazi kwamba hukumu hiyo itakuwa kali sana. Lakini kwa mazao, yaani wanaomcha Mungu, kuna matumaini ya baadaye. Inakuja siku ya haki na uponyaji na furaha. Siku ambapo kwenu ninyi mnaolicha jina langu [= jina la Bwana wa majeshi],jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake; nanyi mtatoka nje, na kucheza-cheza kama ndama wa mazizini (m.2) Siku ambapo Yesu Kristo atakuja kulichukua kanisa lake. Ujumbe wa Agano Jipya utatusaidia kujiandaa kwa siku hiyo, maana akaja kwanza Yohana Mbatizaji, kisha akaja Yesu, kama Bwana alivyoahidi, Nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya. Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana (m.5-6). Zaidi ya hayo kuna kuna habari ya mashahidi wawili kuwepo siku za mwisho kabla Yesu hajaja kwa nguvu na utukufu mwingi, na matendo ya mashahidi hawa hufanana na alivyofanya nabii Eliya: Hao wana amri ya kuzifungu mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao (Ufu 11:6).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mithali, Yohana na Malaki. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/