Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano
Paulo anaonyesha kusudi la Mungu kuweka sheria. Sheria siyo suluhisho la matatizo yote ya dhambi. Anasema, Siibatili neema ya Mungu; maana, ikiwa haki hupatikana kwa njia ya sheria, basi Kristo alikufa bure (2:21). Badala yake, sheria iliwekwa kuwa mwongozo mpaka atakapofika Kristo. Kwa njia ya imani katika Kristo, Mungu anatuonyesha kanuni ya haki ambayo utakatifu wake unadai: Hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa imani (3:11). Ufahamu huu wa sheria unavuka mipaka ya ukabila, jinsia na utamaduni. Hivi vyote ni muhimu, lakini si lazima katika uhusiano wetu na Kristo, maana kila anayemwamini amekuwa mrithi katika ufalme wa Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mithali, Yohana na Malaki. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/