Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

SIKU 30 YA 31

Kwamba watu wamtolee Mungu nao watabarikiwa, ni mafundisho ya hatari, kwani watu wanaoelewa vibaya wanataka kuona mara moja mafanikio baada ya kutoa kwao. Wasipoona baraka, hukoma kumtolea Mungu. Hapo wanaomcha Mungu wanapaswa kufarijiana, wakikumbushana kwamba Mungu amekwisha wabariki, na wanapotoa ni kama wanaonyesha shukrani zao kwake. Hatatusahau kamwe! Katika siku ya Bwana atatupokea kwake: Watakuwa wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye (m.17). Basi, tuendelee kumwamini Mungu na ahadi zake hata katika magumu pasipo kukata tamaa.

siku 29siku 31

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha