Maelezo ya mpango
Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano
![Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F34662%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
"Nirudieni mimi", asema Bwana. Wito huu unaelezana na wito mwingine katika m.10, "Leteni zaka kamili". Maana ya kumrudia Bwana ni sisi kwenda kwake pamoja na vyote tulivyo navyo, pia zaka. Na ahadi katika m.10 juu ya kubarikiwa na Mungu si namna ya mapatano ya kibiashara kwamba ukinipa 10 % nitakupa 20 %. Baraka kuu ni kwamba Bwana ataturudia sisi, kama anavyosema katika m.7, Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi. Hii ni neema yake ya ajabu ambayo hatustahili. Na ambapo Mungu yupo, zipo pia baraka zake zote. Basi, tumtolee kwa moyo, nasi tutabarikiwa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F34662%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma...
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/