Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano
Israeli wanalalamika kuwa Mungu hawatendei haki kwani wao kama taifa lake hawapati mafanikio wakati mataifa mengine yasiyofanya bidii kushika sheria wanafanikiwa kuliko wao. Jibu la Mungu ni unabii juu ya Yohana Mbatizaji na Kristo Yesu. Kuhusu Yohana Mungu anasema, Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu (3:1a). Na kuhusu Kristo Yesu, angalia kwamba kwanza Mungu anasema “mbele yangu”, kisha anaendelea kusema, Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja (3:1b). Kwanza yeye ataleta ibada takatifu (m.3, Watamtolea Bwana dhabihu katika haki), na baadaye hukumu ya haki itafanyika (m.5, Nitawakaribieni ili kuhukumu). Mungu anavyotaka kwetu ni tuendelee kumtegemea na kutakaswa naye ili tutafute mafanikio toka kwake, maana faida ya vitendo vya uovu si ya kudumu.
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mithali, Yohana na Malaki. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/