Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

SIKU 27 YA 31

Taifa la Mungu lilikosa uaminifu. Wanaume wa Kiyahudi walioa wake wa kigeni wasio Wayahudi, pia waliwapa talaka wake zao. Ingawa wanaendelea kumwabudu Mungu, hapokei sala na sadaka zao, maana wamevunja agano lake: Je! Sisi sote hatuna Baba mmoja? Mungu aliyetuumba siye mmoja tu? Basi, mbona kila mmoja wetu anamtenda ndugu yake mambo ya hiana, tukilinajisi agano la baba zetu? (m.10-11). Mungu atachukua hatua kali dhidi yao, atamtenga mtu atendaye hayo (m.12), maana ndoa si jambo la kimwili tu. Talaka ambayo huleta madhara kwa familia nzima na hasa watoto, huleta vilevile madhara kwa maisha ya kiroho. Tujihadhari roho zetu, maana Bwana achukia kuachana!

siku 26siku 28

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mithali, Yohana na Malaki. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/