Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

SIKU 24 YA 31

Mistari hii inathibitisha hoja ya kumcha, kumheshimu na kumtolea sadaka BWANA, hoja inayopatikana katika m.6-10 (ukiwa na nafasi, ni vizuri kuirudia). Tunajifunza kuwa hata tukimdharau Mungu katika maisha yetu, bado jina la Mungu litaendelea kutukuzwa, maana ukuu wa jina lake hautegemei ushuhuda toka kwa wanadamu, bali hushuhudiwa na matendo ya Mungu mwenyewe. Katika m.11 tunasoma, Tokea maawio ya jua hata machweo yake jina langu ni kuu katika Mataifa; na katika kila mahali unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa jina langu; maana jina langu ni kuu katika Mataifa, asema Bwana wa majeshi. Huu ni unabii juu ya Kanisa la Kikristo. Israeli, taifa teule la Mungu, walikataa kumshuhudia na kumheshimu Mungu (m.12, Ninyi mnalitia [jina langu] unajisi ... nyama yake [Meza ya Bwana] hudharauliwa). Basi, Mungu alileta mataifa mbalimbali wasio Wayahudi katika ufalme wake wanaoendelea kumtukuza na kumheshimu.

siku 23siku 25

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha