Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano
Mambo hayo nataka uyanene kwa nguvu, ili wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Hayo ni mazuri, tena yana faida kwa wanadamu. Lakini maswali ya upuzi ujiepushe nayo(m.8-9). Mambo hayo anayotakiwa kunena ni mambo gani?1.Kwamba tumeokolewa na Mungu bila sisi kustahili. Ndivyo upendo na neema yake ilivyo (m.3-5, 7).2.Kwambatumezaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu(m.5b-6).3. Kwamba tumefanywa warithi wa uzima wa milele (m.7). Tusichoke kunena haya kwa nguvu hata leo!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/