Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

SIKU 1 YA 30

Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia(m.24). Mji wa Yerusalemu uliangamizwa na Warumi mwaka 70 BK. Ndipo ulikuwa unatawaliwa na Mataifa mpaka taifa la Israeli liliposhinda vita ya mwaka 1967. Tangu hapo umetawaliwa tena na Wayahudi. Hii ni dalili kubwa kwamba kurudi kwa Yesu kumekaribia sana. Bado taifa la Israeli halijamkiri Yesu kama Masihi. Ila siku hizi kuna maelfu ya Wayahudi katika ulimwengu mzima wanaomgeukia Yesu! Kutimia kwa Rum 11:25-27 kwamba ...Israeli wote wataokoka... ni karibu!

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/