Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano
Ndugu msomaji, uizingatie sana hotuba hii ya Yesu kuhusu siku za mwisho. Tafadhali ujiweke tayari!Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe(m.33). Ni mambo makubwa na magumu yatakayotokea. Utakuwaje wakati ambaponguvu za mbinguni zitatikisika(m.26)? Je, mwezi utaanza kurukaruka? Nyota zitazimika? Habari hizi hutisha. Lakini kwa Mkristo ni dalili nzuri sana ya Mwokozi wake mpendwa kurudi katika wingu na nguvu na utukufu mwingi! Tafakari zaidi Mkristo anavyohimizwa kufanya:Changamkeni(m.28) –jiangalieni(m.34) –kesheni(m.36)! Ni vizuri kurudia mistari iliyotajwa ili kupata kujua maana yake yote.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/