Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano
Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki … katika dhiki akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini(m.42, 44). Yesu ametangaza kifo chake mara tatu:1)Akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, na kuuawa na siku ya tatu kufufuka(9:22),2)Yashikeni maneno haya masikioni mwenu, kwa kuwa Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu(9:44), na3)Kwakuwa atatiwa mikononi mwa Mataifa, atafanyiwa dhihaka; atatendwa jeuri, na kutemewa mate; nao watampiga mijeledi, kisha watamwua(18:32-33).Hata hivyo si jambo rahisi kwa Mwokozi wetu mpendwa kwenda njia hii! Mbele yake kuna mateso makali kupita kiwango. Katika m.37 amesema itatimia kama ilivyoandikwa kuhusu yeye kwambaalihesabiwa pamoja na wahalifu. Kutendewa kama mhalifu hutisha. Ila mzigo mkubwa zaidi ni dhambi zetu.Atapigwa na Mungu, na kuteswabadala yetu ili sisi tupate kupona (Isa 53:4-6)! Je, umemshukuru?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/