Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

SIKU 5 YA 30

Tatizo la mitume ni la kawaida kwa sisi wanadamu! Twataka kuwa wakubwa, na tukishapata ukuu hutaka kuutumia kwa ajili ya kuwatawala wengine na kujinufaisha wenyewe. Yesu hataki tabia hii iwepo katika kanisa lake anatakaaliye mkubwa ... awe kama aliye mdogo; na mwenye kuongoza kama yule atumikaye(m.26)! Mwenyewe ni mfano bora (ukiwa na nafasi, linganisha m.26-27 inayomwonyesha Yesu kama mtumishi na Yn 13:3-17 ambapo Yesu aliwanawisha miguu wanafunzi wake na kuwaambia kwamba hawana budi kunawishana kama alivyo wanawisha). Tuufuate mfano wa Yesu, hata kama watu watatudharau! Vilevile m.28 hutukumbusha kuwa kutumikia na kuteseka ni sehemu ya kuwa mfuasi wa Yesu:Nanyi ndinyi mliodumu pamoja nami katika majaribu yangu.Yule atakayekuwa mwaminifu hadi kufa, atakwezwa na Yesu atakapokuja, na ataketipamoja na Baba ... katika kiti chake cha enzi(Ufu 3:21).

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/