Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

SIKU 4 YA 30

Huu ni mwanzo wa mlo ule uitwao ”Meza ya Bwana.” Ili kusherehekea Pasaka siku hizi, huwa tunakula chakula kizuri kuliko kawaida tukisema, ”Tumekula pasaka.” Ni desturi nzuri. Huenda wengine hawafurahi sana kwa vile wameshindwa kuandaa chakula kizuri, ila tusisahau kwamba kwa Mkristo, maana ya kwanza ya ”kula pasaka” ni kushiriki kwenye Meza ya Bwana. Yesu ana hamu sana kushirikiana nawe anasema,Nimetamani sana kuila pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu(m.15). Kwa mlo huu anathibitisha kuwa tunasamehewa dhambi kwa ajili ya yeye kujitoa msalabani. Ndiyo maana yake kusema,Kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi(Mt 26:28)!

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/