Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano
Tangu sasa Mwana wa Adamu atakuwa ameketi upande wa kuume wa Mungu Mwenyezi. Wakasema wote, Basi, wewe ndiwe Mwana wa Mungu?(m.69-70). Mara nyingi Yesu alikuwa amejiita ”Mwana wa Adamu”. Walijua kwamba jina hili limetoka katika unabii wa nabii Danieli unaomhusu Masihi. Danieli alitabiri hivi,Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa(Dan 7:13-14). Unabii huu unaonyesha kwamba Masihi atakuwa mfano wa mwanadamu na kwamba atakuwa karibu na Mungu (”mzee wa siku”) na kupewa mamlaka yote. Yesu anathibitisha kwamba yeye ndiye mtu huyo, yaani, Mwana wa Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/