Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano
Je, wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi(m.39). Askari na wale wakuu wa Wayahudi pia walimtukana Yesu hivyo wakisema,Aliokoa wengine; na ajiokoe mwenyewe, kama ndiye Kristo wa Mungu, mteule wake(m.35). Tena wakesema,Kama wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi, ujiokoe mwenyewe(m.37). Waliona Yesu kushindwa kujiokoa ni dalili wazi kwamba yeye si Masihi, bali ni mdanganyifu. Hawakutambua kwamba Yesu alifanya hayo kwa hiari na kwa ajili yao. Je, wewe umetambua? Omba msaada wa Roho Mtakatifu usomapo Maandiko ili upate kuona! Mhalifu wa pili aliokoka, maana1) alikubali makosa yake, na2) kujikabidhi kwa Yesu kwa imani. Hata dhambi zake Yesu alizichukua.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/