Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano
Leo ni siku kubwa sana ulimwenguni mwote. Siku ya Pasaka ni siku ya kukumbuka Yesu Kristo alivyofufuka baada ya kukaa kaburini siku tatu. Kufufuka kwa Yesu ni muujiza mkubwa kuliko yote na siri ya nguvu zetu kama Wakristo. Tutumie siku hii kumshukuru Mungu na kwenda kwa wasioamini kushuhudia nguvu za ufufuo. Wanawake walitangaza:Yesu amefufuka katika wafu; halafu waliwaambia wenzao waende wapi ili kumwona. Tufanye vivyo hivyo. Leo Yesu anakutana nasi kwa njia ya Neno lake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/