Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

SIKU 22 YA 30

Akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko(m.45). Hatuwezi kamwe kuelewa Biblia bila kufunuliwa na Yesu. Kwa hiyo tuwe wanyenyekevu tusomapo Biblia au kusikiliza mahubiri; tuwe tunaomba. Hasa wewe unayehubiri Neno la Mungu, usisahau kupiga magoti unapojiandaa ili upate kuongozwa na Roho Mtakatifu! Na tusisahau kwamba yale mengi Yesu aliyowafunulia mitume siku zile baada ya kufufuka, wameyaandika katika Agano Jipya! Ndivyo Yesu alivyoahidi kufanya akisema:Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa. Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote(Yn 16:12). Sasa walijua Yesu kweli yu hai, wakafurahi mno wakimsifu Mungu (m.52-53,Wakamwabudu; kisha wakarudi Yerusalemu wenye furaha kuu. Nao walikuwa daima ndani ya hekalu, wakimsifu Mungu)! Wewe, je?

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/