Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

SIKU 26 YA 30

Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia(m.15). Ukichukua mstari huu peke yake ulivyo na kuufanyia kazi bila kuangalia mafundisho yote ya Paulo katika somo la leo, utapotoka. "Vitu vyote"kwa hapa inamaanisha hasa chakula. Maana zile hadithi na maagizo ya Kiyahudi anayotaja katika m.14 yalihusu hasa chakula (maneno yenyewe yanasema,Wasisikilize hadithi za Kiyahudi, wala maagizo ya watu wajiepushao na yaliyo kweli). M.15 unasema,Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao.Ili kuelewa zaidi linganisha na Mk 7:1-23 na hasa m.14-23 yanayosema: Yesuakawaita makutano tena, akawaambia, Nisikieni nyote na kufahamu. Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu. Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie.] Hata alipoingia nyumbani, ameuacha mkutano, wanafunzi wake wakamwuliza habari za ule mfano. Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi; kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote. Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi. Ukiwa na nafasi, soma pia 1 Tim 4:1-5 na Rum 14:14, 20.

siku 25siku 27

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/