Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano
Tunaweza kugawa mistari ya leo katika sehemu tatu:1. Ombi la kusamehewa na Bwana.Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako, Unisamehe uovu wangu, maana ni mwingi(m.11).2. Bwana ana ushirikiano wa karibu na yeye amchaye.Ni nani amchaye Bwana? Atamfundisha katika njia anayoichagua. Nafsi yake itakaa hali ya kufanikiwa; Wazao wake watairithi nchi. Siri ya Bwana iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake(m.12-14).3. Ombi kwa Bwana la kumwokoa na adui zake na dhambi yake.Uniangalie na kunifadhili, Maana mimi ni mkiwa na mteswa. Katika shida za moyo wangu unifanyie nafasi, Na kunitoa katika dhiki zangu. Utazame teso langu na taabu yangu; Unisamehe dhambi zangu zote. Uwatazame adui zangu, maana ni wengi, Wananichukia kwa machukio ya ukali. Unilinde nafsi yangu na kuniponya, Nisiaibike, maana nakukimbilia Wewe. Ukamilifu na unyofu zinihifadhi, Maana nakungoja Wewe(m.15-22).Katika shida za moyo wangu unifanyie nafasi(m.17). Huenda shida yako ni katika kuchagua elimu, kupata mwenzi au kupata shamba zuri. Basi, soma na uone ahadi ya Mungu kwako:Ni nani amchaye Bwana? Atamfundisha katika njia anayoichagua. Nafsi yake itakaa hali ya kufanikiwa; Wazao wake watairithi nchi. Siri ya Bwana iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake!(m.12-14).Msingi wa kuweza kuongozwa na Bwana ni kuishi katika msamaha wa dhambi(m.18 na 8-11)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/