Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

SIKU 25 YA 30

Barua hii iliandikwa na Paulo alipokuwa kwenye safari ya nne ya misioni, kabla hajawekwa kifungoni Rumi kwa mara ya pili. Huenda iliandikwa mwaka 63 (Paulo aliuawa Rumi mwaka 64). Nibarua ya kiuchungaji, yaani imeandikwa kwa Tito, kiongozi wa kanisa, ili:1.Kumtia moyo na kumwelekeza namna ya kuwafundisha na kuwaongoza Wakristo.2. Kumfundisha mwenendo unaofaa kwa kiongozi wa kanisa na kumhimiza mwenyewe awe mfano! Mzee wa kanisa na askofu kwa wakati ule ni kitu kimoja. Ndivyo wanavyotajwa katika Agano Jipya. tusome mistari hii kupata mfano:Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru(m.5).Maana imempasa askofu awe mtu asiyeshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa MUNGU; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mlevi wala mgomvi, asiwe mpenda mapato ya aibu(m.7). Linganisha habari hizo na Mdo 20:17 na 28:Toka Mileto Paulo akatuma watu kwenda Efeso, akawaita wazee wa kanisa. –Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.

Andiko

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/