Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

SIKU 28 YA 30

Imesemekana kwamba mchungaji mmoja aliwaambia Wakristo: "Myafuate yale ninayosema, lakini msifuate ninayotenda." Msimamo kama huu umepotoka, na ni kinyume kabisa cha neno la leo. Neno lasema k.mf.:Katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema(m.7)... wayapambe mafundisho ya Mwokozi wetu Mungu katika mambo yote(m.10).Neno linatukumbusha tena kuwa,ikiwa mtu hakushitakiwa neno, naye ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni wafisadi wala wasiotii. Maana imempasa askofu awe mtu asiyeshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa MUNGU; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mlevi wala mgomvi, asiwe mpenda mapato ya aibu. bali awe mkaribishaji, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kudhibiti nafsi yake(1:6-8). Kiongozi asipokuwa na mwenendo unaopatana na mafundisho yake, anampa yule mwovu nafasi ya kujiinua. Kwa hiyo katika m.8 tunaambiwa tuyashikemaneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu. Je, umelitii agizo hili?

siku 27siku 29

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/