Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 25:11-22

Zab 25:11-22 SUV

Ee BWANA, kwa ajili ya jina lako, Unisamehe uovu wangu, maana ni mwingi. Ni nani amchaye BWANA? Atamfundisha katika njia anayoichagua. Nafsi yake itakaa hali ya kufanikiwa; Wazao wake watairithi nchi. Siri ya BWANA iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake. Macho yangu humwelekea BWANA daima, Naye atanitoa miguu yangu katika wavu. Uniangalie na kunifadhili, Maana mimi ni mkiwa na mteswa. Katika shida za moyo wangu unifanyie nafasi, Na kunitoa katika dhiki zangu. Utazame teso langu na taabu yangu; Unisamehe dhambi zangu zote. Uwatazame adui zangu, maana ni wengi, Wananichukia kwa machukio ya ukali. Unilinde nafsi yangu na kuniponya, Nisiaibike, maana nakukimbilia Wewe. Ukamilifu na unyofu zinihifadhi, Maana nakungoja Wewe. Ee Mungu, umkomboe Israeli, Katika taabu zake zote.