Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 25:11-22

Zaburi 25:11-22 SRUV

Ee BWANA, kwa ajili ya jina lako, Unisamehe uovu wangu, maana ni mwingi. Ni nani amchaye BWANA? Atamfundisha katika njia anayoichagua. Watafanikiwa maishani mwao; Na wazawa wao wataimiliki nchi. Siri ya BWANA iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake. Macho yangu humwelekea BWANA daima, Naye atanitoa miguu yangu katika wavu. Uniangalie na kunifadhili, Maana mimi ni mkiwa na mteswa. Uniondolee shida za moyo wangu, Na kunitoa katika dhiki zangu. Utazame mateso yangu na taabu yangu; Unisamehe dhambi zangu zote. Uwatazame adui zangu, maana ni wengi, Na kwa namna wanavyonichukia kwa ukatili mwingi. Unilinde nafsi yangu na kuniokoa, Usiniache niaibike, maana nakukimbilia Wewe. Ukamilifu na unyofu zinihifadhi, Maana nakungoja Wewe. Ee Mungu, umkomboe Israeli, Katika taabu zake zote.

Soma Zaburi 25