Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano
Ni wazi kwamba zaburi hii ni ombi la mtu wa Mungu akiwa taabuni. Hata Wakristo wakati mwingine tunaingia katika taabu ambayo inatukwamisha, k.mf. dhambi fulani au kuudhiwa kwa ajili ya imani yetu. Ndipo inatufaa tuombe sala hii! Mistari ya leo ina sehemu nne:1. Kumtumaini Bwana taabuni.E Bwana, nakuinulia nafsi yangu, Ee Mungu wangu, Nimekutumaini Wewe, nisiaibike, Adui zangu wasifurahi kwa kunishinda.
Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja; Wataaibika watendao uhaini bila sababu(m.1-3).2. Ombi la kuongozwa na Bwana.Ee Bwana, unijulishe njia zako, Unifundishe mapito yako, Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa(m.4-5).3. Ombi la kusamehewa na Bwana.Ee Bwana, kumbuka rehema zako na fadhili zako, Maana zimekuwako tokea zamani. Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu, Wala maasi yangu. Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako, Ee Bwana kwa ajili ya wema wako(m.6-7).4. Kufundishwa njia ya Bwana (m.8-10).Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja(m.3). Rum 8:31-39 huthibitisha hiyo kwa msisitizo huu,Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu? ... Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki. Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea. Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? ... Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/