Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

SIKU 21 YA 30

Amani iwe kwenu(m.36). Maneno hayo yameandikwa mara nne tu katika Agano Jipya, na kila mara ayanenaye ni Yesu. Yanapatikana pia katika Yn 20:19, 21 na 26. Ni salamu yake pekee baada ya kufufuka kwake. Yamaanisha kwamba sasa kuna amani kati ya Mungu na wanaopokea maneno hayo ya Yesu. Deni la dhambi zao limekwisha lipwa, damu ya Yesu ilipomwagika msalabani, maanakwa kupigwa kwake sisi tumepona(Isa 53:5).Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba. Akaja akahubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali, na amani kwao wale waliokuwa karibu. Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja(Efe 2:13-18). Kwa kumfufua Yesu, Mungu ameonyesha kwamba ameukubali kabisa upatanisho huo! Kitambulisho cha Yesu ni alama za vidonda vyake mwenyewe. Anaonyesha utambulishohuu akisema,Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo. Na baada ya kusema hayo aliwaonyesha mikono yake na miguu yake(m.39-40).

siku 20siku 22

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/