Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano
Hawakuwasadiki(m.12). Wanafunzi walikuwa wazito kuamini neno la Yesu. Ameshawaambia kwamba atatiwa mikononi mwa Mataifa,nao watampiga mijeledi, kisha watamwua; na siku ya tatu atafufuka(18:33). Wameona jinsi neno lake kuhusu mateso na kifo lilivyotimizwa. Hata hivyo wamesahau maneno yake mengine kuhusu kufufuka baada ya siku tatu. Kwa hiyo katika somo la leo tunaona jinsi walivyokumbushwa juu ya habari hizo:Kumbukeni alivyosema nanyi alipokuwa akaliko Galilaya, akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kutiwa mikononi mwa wenye dhambi, na kusulibiwa, na kufufuka siku ya tatu. Wakayakumbuka maneno yake(m.6-8). Hata wanawake walipowashuhudia mitume hawakusadiki. Je, wewe umeamini na kumsifu Mungu? Usiendelee kuishi kana kwamba Yesu bado yu mfu. Zingatia swali katika m.5:Kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu?Yesu yu hai! Umkaribishe moyoni mwako. Umkabidhi maisha yako kila siku. Naye atakushirikisha ushindi wake sasa na hata milele! Haleluya!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/