Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano
Yule akida alipoona yaliyotukia, alimtukuza Mungu, akisema, Hakika yake, mtu huyu alikuwa mwenye haki(m.47). Ni matukio gani yaliyomfanya huyu askari (jemadari) kutambua hilo? 1. Alisikia baadhi ya maneno ya Yesu, kwa mfano aliposema,Baba,uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo(m.34) na alipomwambia mharifu msalabani akisema,Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi(m.43).2. Kwa masaa matatu wakati wa mchana palikuwa na giza juu ya nchi yote (dunia nzima).3. Nchi ilitetemeka na miamba ikapasuka (Mt 27:51,Na tazama, pazia la hekalu kikapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka). – Ni siku yenye matukio ya pekee sana katika historia ya binadamu. Kwa hiyo Mungu alitaka hata uumbaji ushuhudie!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/