Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano
Siku ya leo ina majina mengi ikiwa ni pamoja naChakula cha BwananaMeza takatifu ya Bwana. Somo linaitazama sakramenti ya Meza ya Bwana kama ushirika, tena ushirika mtakatifu, maana ni shirika na Yesu. Ni ushirika huu Yesu aliomwambia Petro akisema,Nisipokutawadha, huna shirika nami(m.8). Tunapaswa kushiriki ili tuendelee kutakaswa na Yesu, na kuhakikishiwa kuhusu upendo wake kwetu. Hivyo tutapata nguvu ya kwenda kumshuhudia Yesu ulimwenguni na kuwatendea watu kwa upendo, kama alivyotutendea.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/