Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

SIKU 11 YA 30

Wayahudi hawakuwa na mamlaka ya kumhukumu mtu kufa bila ruhusa ya Pilato. Ni sababu ya hao kuendelea kumdai. Mara nne Pilato anasema Yesu hajafanya kosa lolote lipasalo kufa. Mara ya kwanza akawaambia,Sioni neno lililo ovu katika mtu huyu(m.4). Halafu akasema,Mtu huyu mmemleta kwangu kana kwamba anapotosha watu; nami, tazama, nimeamua mambo yake mbele yenu, ila sikuona kwake kosa lo lote katika mambo hayo mliyomshitaki; wala hata Herode, kwa maana amemrudisha kwetu; basi tazama, hakuna neno lo lote alilolitenda lipasalo kufa(m.14-15). Akawauliza kwa mara nyingine,Mtu huyu mmemleta kwangu kana kwamba anapotosha watu; nami, tazama, nimeamua mambo yake mbele yenu, ila sikuona kwake kosa lo lote katika mambo hayo mliyomshitaki; wala hata Herode, kwa maana amemrudisha kwetu; basi tazama, hakuna neno lo lote alilolitenda lipasalo kufa(m.22). Na wakitaka awafungulie Baraba ambaye ni mwuaji, anakubali. Maana walisisitiza wakisema,Mwondoe huyu, utufungulie Baraba(m.18). Hiyo inaonyesha wazi kwamba Pilato anapenda zaidi kubaki madarakani kuliko kutenda haki. Ilivyotokea kwa Baraba ni mfano wa wewe na mimi. Sisi ni wenye dhambi, tumestahili kufa. Lakini Yesu alikufa badala yetu ili sisi tusamehewe na kuwa huru. Bwana asifiwe!

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/