Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

SIKU 9 YA 30

Mfalme Herodeakamwuliza maneno mengi, yeye asimjibu lo lote(m.9). Yesu alikuwa kimya kabisa.Wakuu wa makuhani na waandishi wakasimama wakamshitaki kwa nguvu sana(m.10). Lakini Yesu hakujitetea, bali alinyamaza tu kama ilivyoandikwa katika Mt 26:62-63:Kisha Kuhani Mkuu akasimama akamwambia, Hujibu neno? Hawa wanakushuhudia nini? ... Yesu akanyamaza.Kwa njia hiyo alitimiza neno lisemalo:Alionewa, lakini alinyenyekea, wala hakufunua kinywa chake; kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, na kama vile kondoo anyamazavyo mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake(Isa 53:7). Pia Yohana Mbatizaji alishuhudia akasema,Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!(Yn 1:29).

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/