Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 08/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 08/2020

SIKU 16 YA 31

Wazee wa Israeli walitafuta ushauri wa Mungu kumpitia nabii, lakini hawakujibiwa neno ila hili moja tu: Rudini(m.6). Je, si walivyofanya? Hapana, wamejikwaa! Kwazo lao ni kwamba wamekubali mioyo yao kutawaliwa na miungu mingine na macho yao kutazama kwa tamaa kitu kile kilichowatenganisha na Mungu (m.3:Mwanadamu, watu hawa wametwaa vinyago vyao na kuvitia mioyoni mwao, nao wameweka kwazo la uovu wao mbele ya nyuso zao. Je! Ni laiki yangu niulizwe na wao katika neno lo lote?Pia katika m.7 imeandikwa kuhusu ajitengaye na Mungu kwamba amefanya hivyo kwa kuvitwaa vinyago vyake na kuvitia moyoni mwake, na kuliweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake). Wasipogeuka, Mungu atashughulikia nao. Kila mtu atachukua uovu wake. Zingatia ilivyoandikwa katika m.11 kuhusu lengo la Mungu akifanya hivyo: ili nyumba ya Israeli wasipotee mbali nami, wala wasijitie unajisi tena kwa makosa yao yote; bali wawe watu wangu, nami niwe Mungu wao, asema Bwana MUNGU. Tujitathmini! Tujiulize ni miungu gani mioyo yetu imeshikilia.

siku 15siku 17

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 08/2020

Soma Biblia Kila Siku 08/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli na 2 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

Mipango inayo husiana