Soma Biblia Kila Siku 08/2020Mfano
Mungu anafafanua uhusiano wake na Waisraeli kwa kutumia mfano wa ndoa na unyumba. Watu wa Mungu wamezini kiroho kwa kuabudu miungu mingine. Hiyo ni maana mfano uliotumika katika m.16-18:Ukatwaa baadhi ya mavazi yako, ukajifanyia mahali palipoinuka, palipopambwa kwa rangi mbalimbali, ukafanya mambo ya kikahaba juu yake; mambo kama hayo hayatakuja wala hayatakuwako.Pia ulivitwaa vyombo vyako vya uzuri, vya dhahabu yangu na vya fedha yangu, nilivyokupa, ukajifanyia sanamu za wanaume, ukafanya mambo ya kikahaba pamoja nazo;ukatwaa nguo zako za kazi ya taraza, ukawafunika, ukaweka mafuta yangu na uvumba wangu mbele yao. Kwa maneno mengine walitegemea mataifa yenye nguvu kuliko Mungu (m.26:Umezini na Wamisri, jirani zako, wakuu wa mwili. Na m.28-29: Pia umefanya mambo ya kikahaba pamoja na Waashuri, kwa sababu ulikuwa huwezi kushibishwa; naam, umefanya mambo ya kikahaba pamoja nao, wala hujashiba bado.Pamoja na hayo umeongeza mambo yako ya kikahaba katika nchi ya Kanaani, mpaka Ukaldayo, wala hujashibishwa kwa hayo). Hawajawa waaminifu kwa sababu mbili: 1.Waliona mafanikio yao yalitokana na juhudi zao wenyewe (m.15: Uliutumainia uzuri wako). 2.Walisahau hali yao ya asili (m.22: Hukuzikumbuka siku za ujana wako, ulipokuwa uchi, huna nguo, ukawa ukigaagaa katika damu yako). Faida yao imekuwa nini? Wamepoteza kila kitu! Ni vizuri tujihoji na kumgeukia Mungu, tusipoteze vilevile uhusiano wetu mwema na Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli na 2 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz