Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 08/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 08/2020

SIKU 22 YA 31

Mungu anamlinganisha mkewe, binti Yerusalemu, na maumbu yake, Samaria na Sodoma. Twajua uovu wa Sodoma, lakini machoni pa Mungu watu wa Yerusalemu wametenda vibaya zaidi kwa kuvunja agano la ndoa na Mungu (m.59: Bwana MUNGU asema hivi; Nitakutenda vile vile kama ulivyotenda, uliyekidharau kiapo kwa kulivunja agano). Kwa nini Mungu analinganisha hivyo? Hafurahii kifo cha mwenye dhambi (18:32: Mimi sikufurahii kufa kwake afaye, asema Bwana MUNGU; basi ghairini, mkaishi), bali ataka kuweka imara agano lake na Waisraeli. Lengo ni watambue uovu wao na kutahayari, na hivyo kumrudia mume wao ili awasamehe, kama Mungu anavyosema katika m.63, Upate kukumbuka, na kufadhaika,usifumbue kinywa chako tena, kwa sababu ya aibu yako; hapo nitakapokusamehe yote uliyoyatenda). Hivyo Mungu anadhihirisha upendo wake na nguvu ya neema yake.

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 08/2020

Soma Biblia Kila Siku 08/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli na 2 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

Mipango inayo husiana