Soma Biblia Kila Siku 08/2020Mfano
Kazi ya kumshuhudia Kristo katika mazingira yetu si ya kikundi fulani au watu maalumu tu. Ili ujumbe wa Injili uwafikie watu wengi na kwa haraka, yatupasa sote tunaomwamini Yesu Kristo tujitoe na tushirikiane katika kumtangaza huyu Mwokozi wa ulimwengu. Tufanye hivyo kwa njia ya kuwa nuru na chumvi kwa siri na kwa wazi. Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni (Mt 5:13-16). Yesu Kristo ametupatia Roho Mtakatifu ili atuwezeshe kusema na kushuhudia kwa nguvu na uweza. Sasa nusu mwaka umekwenda, umeshawaleta wangapi kwa Yesu Kristo? Zingatia maswali yafuatayo:Wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema! (Rum 10:14-15)
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli na 2 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz