Soma Biblia Kila Siku 08/2020Mfano
![Soma Biblia Kila Siku 08/2020](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F21080%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Kuwa mfuasi wa Kristo si jambo la siri au kificho. Mkristo ni kama ubao wa matangazo. Ubao huu unasomwa na watu wote. Hatari yetu ni kuharibu au hata kuchafua yaliyoandikwa ubaoni au barua hii. Matokeo ya kuonekana kwetu ni kumwinua Kristo. Ulimwengu utatambua kuwepo kwa Kristo kwa njia ya ushuhuda wetu. Je, unasomekaje mbele ya jirani zako? Rudia mistari mitatu ya kwanza ya somo la leo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku 08/2020](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F21080%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku 08/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli na 2 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz