Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 08/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 08/2020

SIKU 25 YA 31

Ujio wa Yesu Kristo katika maisha yetu unaleta maisha ya kuishi kwa kuamua. Maazimio haya ni ya kumfuata, kumkiri, kumwamini na kumtegemea Yesu Kristo. Uamuzi huu, ndio unaotuwezesha kuishi na kufuata utakatifu wa Yesu Kristo. Ahadi za Yesu Kristo haziambatani na dhambi wala ukengeufu. Zingatia k.m. ilivyoandikwa katika mistari ifuatayo: Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu(1 Pet 3:18). Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu(Ebr 2:9). Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu.Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi(Ebr 4:14-15). Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea(Rum 8:34). Kumfuata Yesu Kristo kunatupatia uhakika wa kuishi kwa uaminifu kama yeye alivyo.

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 08/2020

Soma Biblia Kila Siku 08/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli na 2 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz